Unyanyasaji ni nini?

Naomba mtu mwenye tafsiri sahihi ya unyanyasaji
Ni ile hali ya kumfanyia mtoto vitendo vya kumkosesha amani na furaha katika maisha yake mfano kipigo kupitiliza,ubakaji,ulawiti,kumpa kazi isiyolingana na umri wake nk
Ni jumla ya mambo yote ambayo kama ukimfanyia mtoto yanatweza utu na ubinadamu wa mtoto.
- 1 amependezwa
Ni hali ya kumfanyia vitendo vinavyoweza kudhuru afya yake kama Kimwili,Kiakili,Kihisia na kijamii
Ni hali ya kumfanyia vitendo vinavyoweza kumuathili mtoto kimwili,kihisia na kiakili
Ni haki na ni jukumu la kila mtu kumlinda na kumtunza mtoto na kijana.
Ni hari ya kumnyima mtoto haki ya uhuru wa kuishi au kujiongoza kutokana na jinsia yake.
Ulinzi wa mtoto ni kumlinda mtoto dhidi ya unyanyasaji wake katika nyanja mbali mbali kama vile unyanyasaji wa kimwili, kingono, kiimani,.kiutamaduni na mengineyo
- 1 amependezwa
Ni vitendo vyooote vinavyofanywa ili kuminya haki ya Mtoto, mf. Kumnyima: chakula, elimu, haki ya kujieleza, kumpiga, haki ya kucheza, n.k
- 1 amependezwa
Ni vitengo vinavyofanywa kwa mtoto na kuwa na matokeo hasi ya makuzi ya kimwili , kiakili, kisaikolojia na kijamii.
Ni jumla ya matendo yote yanayoweza kumuathiri Mtoto Kimwili, Kiakili, Kihisia na Kijamii. Mfano Kumpiga, Kumnyima chakula, Kumchoma moto mikono n.k
- 1 amependezwa