Kama mshiriki wa familia ya kimataifa ya Compassion, wewe ni mtetezi wa watoto na vijana, hata kama hufanyi kazi nao moja kwa moja. Katika kozi hii husika, utajifunza jinsi ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji, kutelekezwa au unyonyaji wa watoto na vijana. Kozi hii inajumuisha uthibitisho wa Kanuni za Maadili za Compassion kuhusu Ulinzi na Usalama wa Watoto na Vijana.
Lengo la mafunzo haya ni kuwapawanafunzi ufahamu na ujuzi wa kukabiliana
na unyanyasaji wa watoto kingono mtandaoni (UWKM). Itarahisisha kutambua ishara
na dalili za UWKM, kuelimisha walengwa juu ya madhara ya muda mrefu ya UWKM,
Kuwasilisha mikakati ya kutekeleza na kuwasaidia wanafunzi kutambua namna
mbalilmbali za kuwaponya wahanga katika mazingira yao.
Lengo la mafunzo haya ni kumwezesha mwanafunzi kuwa na taarifa naujuzi
wa kushughuikia utelekezaji wa mtoto. Mafunzo haya yataimarisha namna ya
kutambua dalili na ishara za utelekezwaji, itaelimisha wasikilizajikuhusu
madhara ya muda mrefu ya utelekezaji, itawakilisha mbinu/mikakati ya kuingilia
kati na itawasaidia wanafunzi kutambua rasilimali mbadala zilizoko kwenye eneo
husika za kusaidia katika uponyaji wa mwathirika.
Lengo la Mafunzo haya ni kuwawezesha wanaojifunza wapate maarifa na
stadi za kushughulika na Unyanayasaji wa mtoto Kihisia. Itasaidia kuimarisha
namna ya kubainisha ishara na dalili za unyanyasaji kihisia, italeta
mbinu/mikakati ya jinsi ya kuingilia kati na kumsaidia huyu anayejifunza
kutambua huduma kwenye jamii husika ili kupata njia mbalimbali za
kuwasaidia wahanga kupona.
Sehemu ya 1 kati ya 2 ya mafunzo kwenye kompyuta ambayo yanawapa wafanyakazi wa kanisa na waliojitiolea uwezo wa kuwasaidia watoto katika jamii zao kupona kutokana na kiwewe.
Ulinzi wa Watoto: Mafunzo ya Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe ni pamoja na kozi mbili kwenye kompyuta na warsha tatu za mtandaoni. Warsha za mtandaoni zitaratibiwa na kusimamiwa na mfanyakazi katika Ofisi za Taifa za Compassion. Ili kupokea cheti kwa ajili ya mafunzo haya, wanafunzi watahitaji kukamilisha vipengele vyote vya mafunzo.
1. Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe, Sehemu ya 1 (Kozi) – Upo Hapa!2. Warsha ya Mtandaoni 1
3. Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe, Sehemu ya 2 (kozi)
4. Warsha ya Mtandaoni 2
5. Warsha ya Mtandaoni 3 – Cheti
Cheti kitatolewa ndani kulingana na ukamilishaji wa kozi kwenye kompyuta na ushiriki katika warsha za mtandaoni.
Sehemu ya 2 kati ya 2 ya mafunzo kwenye kompyuta ambayo yanawapa wafanyakazi wa kanisa na waliojitiolea uwezo wa kuwasaidia watoto katika jamii zao kupona kutokana na kiwewe.
Ulinzi wa Watoto: Mafunzo ya Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe ni pamoja na kozi mbili kwenye kompyuta na warsha tatu za mtandaoni. Warsha za mtandaoni zitaratibiwa na kusimamiwa na mfanyakazi katika Ofisi za Taifa za Compassion. Ili kupokea cheti kwa mafunzo haya, wanafunzi watahitaji kukamilisha vipengele vyote vya mafunzo.
1. Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe, Sehemu ya 1 (kozi)2. Warsha ya Mtandaoni 1
3. Utunzaji wa Kwanza Baada ya Kiwewe, Sehemu ya 2 (Kozi) <--*Upo Hapa!*
4. Warsha ya Mtandaoni 2
5. Warsha ya Mtandaoni 3 – Cheti
Cheti kitatolewa ndani kulingana na ukamilishaji wa kozi kwenye kompyuta na ushiriki katika warsha za mtandaoni.