Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue nyenzo/raslimali zilizomo. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | RASLIMALI ZA KUFUNDISHIA WATOTO NA VIJANA > MAENDELEO YA KIROHO > Mtaala wa Kiroho 3-5 |
Copyright Owner | Compassion International |
Mtaala huu umetayarishwa kwa ajili ya watoto wa umri miaka 3-5. Unahusisha masomo yatakayosaidia kumjenga mtoto kiroho. Masomo yaliyomo ni: kuifahamu na kuijua Biblia, kufahamu na kujua masimulizi ya historia katika Biblia, kutambua kwamba Mungu alimuumba mwanadamu na vitu vyote vilivyo duniani, kujua matukio makuu katika Agano la Kale na Agano Jipya, kutambua kwamba Yesu ni mwokozi wa ulimwengu na aliwapa wanafunzi wake kazi ya kuhubiri habari njema kwa watu wote, Yesu alienda mbinguni na atarudi tena duniani. Kila mojawapo ya masomo haya arobaini na sita yanahusisha mpangilio wa somo (Urefu, matayarisho na vifaa vya kutumia). Muda wa darasa, unaohusisha maelezo kwa kina, jinsi ya kufundisha, pamoja na michezo na shughuli zinazowashirikisha wanafunzi ili kuwasaidia kusoma na kuelewa. Kuna tathmini ya mwalimu na ya mwanafunzi pia. Masomo na shughuli za vitendo zinadhamiriwa kutumiwa kwa makundi.
Mtandao wa ForChildren.com unatolewa na shirika la Compassion International, shirika lisilo la faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.