Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue nyenzo/raslimali zilizomo. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | RASLIMALI ZA KUFUNDISHIA WATOTO NA VIJANA > MAENDELEO YA KIAKILI > Mtaala wa Kiakili 3 - 5 |
Copyright Owner | Compassion International |
Mtaala huu ni kwa ajili ya watoto wa miaka 3-5. Unahusisha masomo arobaini na mbili, yatakayosaidia kumjenga mtoto kiakili. Masomo yatahusisha mada kama: kujitambua mimi ni nani, rangi na maumbo, uundaji wa vitu, kuielewa jamii yangu, chakula ninachokula hutoka wapi, ulimwengu wa kazi, naweza kusimulia hadithi, siku za mapumziko/sherehe. Kila mojawapo ya masomo haya arobaini na mbili yanahusisha mpangilio wa somo (urefu, matayarisho na vifaa vya kutumia). Muda wa darasa, unaohusisha maelezo kwa kina, jinsi ya kufunza, pamoja na michezo na shughuli zinazowashirikisha wanafunzi ili kuwasaidia kusoma na kuelewa. Kuna tathmini ya mwalimu na ya mwanafunzi pia. Masomo na shughuli za votendo zinatazamiwa kutumika kwa makundi.
Mtandao wa ForChildren.com unatolewa na shirika la Compassion International, shirika lisilo la faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.