Kutuhusu

Tuko kwa ajili ya watoto

Sisi ni wafuasi wa Yesu, tuonaamini kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kutunzwa, kulindwa, na kulelewa. Jambo la  kusikitisha ni kwamba mamilioni ya watoto hao wanateseka na wako katika mazingira hatarishi. Kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini mkubwa duniani kote.[1]   Pamoja na kuwahudumia na watu walio katika hali hatarishi,Yesu pia alionesha mfano wa kutufundisha kwamba watoto wanahitaji kujumuishwa, kulindwa, na kupendwa. Alikuwa upande wa watoto, na kwa hiyo sisi pia tunapaswa kuwa upande wa watoto.

Tunaamini kwamba ustawi wa familia, jamii na kanisa kwa siku za baadaye,  unategemea jitihada tunazofanya sasa za kuzingatia ukuaji  wa watoto katika ujumla wake.  Hivyo, Compassion iko kwa ajili ya  kuimarisha uwezo wa makanisa ili kutoa usaidizi fanisi wa ukuaji wa watoto katika ujumla wake kwa kuangalia zaidi wale walio katika umaskini.

ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, inajaribu kuunda jamii ya wafuasi wa Yesu waliojitolea kuwatoa watoto kutoka  kwenye umaskini, waumini ambao wako tayari kusaidia,  kushirikisha ujuzi, mbinu, uzoefu na mawazo ambayo kila mmoja wetu anayo ili kusaidia watoto walio katika umaskini.

Tunakualika ujiunge nasi katika jamii yenye ushirikiano ili  ushirikishe mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.

[1] Olinto, P., Beegle, K., Sobrado, C., & Uematsu, H. (2013). Hali ya Watu Maskini: Maskini wako wapi, Ni wapi pagumu zaidi kumaliza umaskini, na Wasifu wa Sasa wa Maskini Duniani Ukoje? Kigezo cha Uchumi, 125. doi:Oktoba 2013