Main Logo
  • Lugha
  • Ingia katika akaunti/Jiunge
  • Jukwaa la majadiliano
  • Jifunze
  • Maktaba

Teua Lugha Unayopenda

  • English
  • Kiswahili
  • Mwanzo
  • Maktaba
  • Jifunze
  • Jukwaa la majadiliano
  • Lugha
  • Ingia katika akaunti/Jiunge

Kutuhusu

Tuko kwa ajili ya watoto

Sisi ni wafuasi wa Yesu, tuonaamini kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kutunzwa, kulindwa, na kulelewa. Jambo la  kusikitisha ni kwamba mamilioni ya watoto wanateseka na wako katika mazingira hatarishi. Kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini mkubwa duniani kote.[1]   Pamoja na kuwahudumia watu walio katika hali hatarishi,Yesu pia alionyesha mfano wa kutufundisha kwamba watoto wanahitaji kujumuishwa, kulindwa, na kupendwa. Alikuwa upande wa watoto, na kwa hiyo sisi pia tunapaswa kuwa upande wa watoto.

Tunaamini kwamba ustawi wa familia, jamii na kanisa kwa siku za baadaye, unategemea jitihada tunazofanya sasa za kuzingatia ukuaji  wa watoto katika ujumla wake.  Hivyo, Compassion iko kwa ajili ya  kuimarisha uwezo wa makanisa ili kusaidia kwa ufanisi ukuaji wa watoto katika ujumla wake kwa kuangalia zaidi wale walio katika umaskini.

Mtandao wa ForChildren.com, unaotolewa na Shirika la Compassion International, unajaribu kutengeneza jamii ya wafuasi wa Yesu inayojitolea kuwatoa watoto kutoka  kwenye umaskini, waumini ambao wako tayari kusaidia,  kushirikisha ujuzi, mbinu, uzoefu na mawazo ambayo ya kila mmoja wetu ili kusaidia watoto walio katika umaskini.

Tunakukaribisha ujiunge nasi katika jamii yenye ushirikiano ili  ushirikishe mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.

[1] Olinto, P., Beegle, K., Sobrado, C., & Uematsu, H. (2013). Hali ya Watu Maskini: Maskini wako wapi, Ni wapi pagumu zaidi kumaliza umaskini, na Wasifu wa Sasa wa Maskini Duniani Ukoje? Kigezo cha Uchumi, 125. doi:Oktoba 2013

Mtandao wa ForChildren.com, unaotolewa na shirika la Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano ili kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya  wafuasi wa Yesu duniani kote, jamii iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakukaribisha ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.

Mtandao wa ForChildren.com unatolewa na shirika la Compassion International, shirika lisilo la faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.

  • Kutuhusu​
  • Wasiliana Nasi
  • Masharti ya Matumizi
  • Faragha