1. ForChildren.com ni nini?
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano ili kusaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio hatarini. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote, iliyojitolea kwa ajili ukuaji wa watoto katika ujumla. Jiunge na taasisi, mashirika yasiyo ya faida, makanisa na watu binafsi walioungana KWA NIABA YA WATOTO.
2. Kwa nini Compassion International ilitengeneza tovuti hii?
Hadi kufikia mwaka 2015, Compassion International iilifikia kuhudumia watoto milioni 1.7 wanaoishi katika umaskini. Hata hivyo, kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini, inakuwaje kuhusu hao wengine wasiofikiwa? Ingawa changamoto ni kubwa kuliko Compassion, siyo kubwa kuliko Kanisa. Kwa kutengeneza ForChildren.com, Compassion inatoa ujuzi, vifaa ili kuunda kundi na huunda eneo kundi la watu wengi zaidi watakaowafikia watoto mahali walipo. ForChildren.com inaruhusu mtu yeyote kushikisha mchango wa mawazo na machapisho kwa ajili ya watoto na vijana. Unaweza kuwasilisha chapisho lako linalozingatia vigezo ambalo litapokelewa na kukaguliwa. Unaweza kupata mrejesho wa chapisho ikiwa l imekubaliwa au "limekataliwa". Ikiwa "limekataliwa", kutakuwa na maelekezo kuhusu jinsi ya kurekebisha na kuwasilisha upya. Baada ya kupokea taarifa kwamba rasilimali "Imeidhinishwa," itaweza kufikiwa kupitia kipengele cha Discover kwenye ForChildren.com.
6. Ninawasilishaje rasilimali nyingi zinazohusiana?
Ikiwa una rasilimali nyingi zinazohusiana kwenye seti, unaweza kuziwasilisha kama mfululizo. Kwenye ukurasa wa Gundua/Discover, bofya kitufe cha "Shirikisha Mfululizo." Kamilisha fomu ya uwasilishaji wa Mfululizo, na ubofye "Wasilisha." Kisha utaelekezwa kwenye ukurasa wa Mfululizo unapoweza kuweka kila rasilimali iliyopo kwenye mfululizo, moja kwa moja.
7. Ninaanzaje Majadiliano ya Muunganisho?
Kwenye kwa ukurasa wa mbele ForChildren.com, bofya Gundua/Discover. Ukurasa wa Muunganisho una orodha ya majadiliano yote yanayoendelea; unaweza kutafuta na kuona kama kuna mtu ambaye tayari amekuwa akizungumza kuhusu mada yako, au unaweza kubofya kitufe kinachosema "Anza Majadiliano" ili unanzishe!
8. Ni wapi pananiwezesha kutazama maelezo yangu mafupi ?
Baada ya kuingia, angalia kwenye ukurasa wa mbele wa ForChildren.com kwa viungo vitatu vyenye rangi ya samawati upande wa juu kulia; kiungo kimoja kitakuwa ni jina lako. Ukibofya kwenye kiungo hicho, kitakupeleka kwenye ukurasa wa maelezo yako mafupi, mahali unapoweza kudhibiti uwasilishaji wako, uendelee kufuata majadiliano unayoshiriki, uweke picha ya maelezo mafupi, ubadilishe nenosiri lako, utazame maktaba zako, na mambo mengine.
9. Nimesahau nenosiri langu. Nifanye nini?
Kwenye ukurasa wa ingia, chini ya sehemu za jina la mtumiaji na nenosiri, bofya kiungo cha rangi ya samawati kinachosema "Umesahau nenosiri lako?" Kitakupeleka kwenye ukurasa unapoweza kuingiza anwani yako ya barua pepe. Tutakutumia barua pepe iliyo na kiungo kitakacho kuruhusu ubadilishe nenosiri lako.
10. Ikiwa ninahitaji msaada au nina maswali ambayo hayajajibiwa, nifanye nini?
Upande wa chini kulia katika ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com, bofya kiungo cha rangi ya kijivu kinachosema "Wasiliana". Unaweza kuwasilisha ujumbe kwenye timu ya ForChildren, na tutawasiliana na wewe baada ya muda mfupi!