1. ForChildren.com ni nini?
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano ili kusaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio hatarini. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote, iliyojitolea kwa ajili ukuaji wa watoto katika ujumla. Jiunge na taasisi, mashirika yasiyo ya faida, makanisa na watu binafsi walioungana KWA NIABA YA WATOTO.
2. Kwa nini Compassion International ilitengeneza tovuti hii?
Hadi kufikia mwaka 2015, Compassion International iilifikia kuhudumia watoto milioni 1.7 wanaoishi katika umaskini. Hata hivyo, kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini, inakuwaje kuhusu hao wengine wasiofikiwa? Ingawa changamoto ni kubwa kuliko Compassion, siyo kubwa kuliko Kanisa. Kwa kutengeneza ForChildren.com, Compassion inatoa ujuzi, vifaa ili kuunda kundi na huunda eneo kundi la watu wengi zaidi watakaowafikia watoto mahali walipo. ForChildren.com inaruhusu mtu yeyote kushikisha mchango wa mawazo na machapisho kwa ajili ya watoto na vijana. Unaweza kuwasilisha chapisho lako linalozingatia vigezo ambalo litapokelewa na kukaguliwa. Unaweza kupata mrejesho wa chapisho ikiwa l imekubaliwa au "limekataliwa". Ikiwa "limekataliwa", kutakuwa na maelekezo kuhusu jinsi ya kurekebisha na kuwasilisha upya. Baada ya kupokea taarifa kwamba rasilimali "Imeidhinishwa," itaweza kufikiwa kupitia kipengele cha Discover kwenye ForChildren.com.
6. Ninawasilishaje rasilimali au machapisho mengi yanayohusiana?
Ikiwa una rasilimali nyingi au machapisho ambayo yako kwa seti zinazohusiana, unaweza kuziwasilisha kama mfululizo au mfuatano. Kwenye ukurasa wa Discover/Gundua, bofya kitufe cha "Shirikisha Mfululizo." Kamilisha fomu ya uwasilishaji wa Mfululizo, na ubofye "Wasilisha." Kisha utaelekezwa kwenye ukurasa wa Mfululizo unapoweza kupakia kila rasilimali iliyopo katika mfululizo.
7. Ninaanzaje Majadiliano katika eneo la "Unganisha"?
Kwenye ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com, bofya Discover/Gundua. Ukurasa wa "Unganisha" una orodha ya majadiliano yote yanayoendelea kutoka kwa watu mbalimbali; unaweza kutafuta na kuona kama kuna mtu ambaye tayari ameandika kuhusu mada yako, au unaweza kubofya kitufe kinachosema "Anza Majadiliano" ili uanzishe mjadala!
8. Ninaweza kuona taarifa zangu fupi katika eneo gani?
Baada ya kuingia, angalia kwenye ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com katika viungo vitatu vyenye rangi ya samawati hafifu upande wa juu kulia; kiungo kimoja kitakuwa jina lako. Ukibofya kwenye kiungo hicho, kitakupeleka kwenye ukurasa wa taarifa zako fupi, mahali unapoweza kudhibiti uwasilishaji wako, uendelee kufuata majadiliano unayoshiriki, upakie picha ya maelezo mafupi, ubadilishe nenosiri lako, utazame maktaba zako, na mambo mengineyo!
9. Nimesahau nenosiri langu. Nifanye nini?
Kwenye ukurasa wa kuingilia (Log in) , chini ya sehemu za jina la mtumiaji na nenosiri, bofya kiungo cha rangi ya samawati kinachosema "Umesahau nenosiri lako?" Kitakupeleka kwenye ukurasa unapoweza kuingiza anwani yako ya barua pepe. Tutakutumia barua pepe iliyo na kiungo kitakachokuruhusu ubadilishe nenosiri lako.
10. Ikiwa ninahitaji msaa au nina maswali ambayo hayajajibiwa, nifanye nini?
Upande wa chini kulia mwa ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com, bofya kiungo cha rangi ya kijivu kinachosema "Wasiliana". Unaweza kuwasilisha ujumbe kwenye timu ya ForChildren, na tutawasiliana na wewe baada ya muda mfupi!