1. UTANGULIZI NA KIBALI CHA MATUMIZI
Karibu katika tovuti hii inayomilikiwa na kuendeshwa na Compassion International . Tafadhali soma Masharti haya ya Matumizi kwa makini kabla ya kutumia Tovuti hii. Kwa kufikia na/au kutumia tovuti unakubali kutii Masharti ya Matumizi bila kikomo au sifa, zinazoweza kubadilishwa mara kwa mara kwa hiari ya kipekee ya Compassion. Ikiwa hukubaliani na Masharti haya ya Matumizi, huwezi kutumia Tovuti hii.
Unakubali kwamba Masharti haya ya Matumizi yenye mazingatio , upokeaji na utoshelevu ambao unayakubali. Mazingatio hayo yanajumuisha, bila kikomo, matumizi yako ya Tovuti na nyenzo na taarifa inayopatikana kwenye Tovuti hiyo.
2. MABADILIKO KWA MASHARTI HAYA YA MATUMIZI
Compassion inahifadhi haki ya kusahihisha au kurekebisha Masharti haya ya Matumizi, wakati wowote na bila ilani ya kabla, kwa kuchapisha toleo lililorekebishwa kwenye Tovuti. Mabadiliko haya yataanza kutumika tarehe ambayo Compassion inachapisha toleo lililorekebishwa kwenye Tovuti. Matumizi yako ya Tovuti baada ya mabadiliko yoyote kama hayo yanajumuisha kukubali kwako kubanwa na Masharti ya Matumizi yaliyorekebishwa.
Ili kukuarifu kuhusu mabadiliko katika Masharti haya ya Matumizi, Compassion itatoa taarifa juu mwa ukurasa huu kwa angalau siku 30 baada ya tarehe mpya ya kuanza kutumika.
Unaweza kufikia toleo la sasa la Masharti haya ya Matumizi wakati wowote kwa kubofya kwenye kiungo kilichowekwa alama ya "Masharti ya Matumizi" chini mwa kila ukurasa wa Tovuti.
3. UVUMBUZI
Tovuti hii, ikiwa ni pamoja na programu na msimbo unaounda na kuendesha Tovuti hii na maudhui yote ya Tovuti hii, kwa mfano, maandishi, makaratasi, nyaraka, mtaala, vitabu, picha, vielelezo, michoro, chenga za sauti, na chenga za video zote zilizochapishwa kwenye Tovuti (kwa ujumla, "Maudhui"), zimelindwa na alama ya baishara, alama ya huduma, umbo la biashara, hakimiliki, hataza, siri ya biashara na sheria zingine za uvumbuzi. Haki zote zilizo kwenye Tovuti hii, ikiwa ni pamoja na haki zote zilizo katika Maudhui, zinamilikiwa na Compassion au watoa leseni wake, na watu wengine wa tatu. Tovuti hii imesajiliwa kama kazi ya jumla chini ya sheria na mikataba ya hakimiliki za Marekani na za kimataifa, na Compassion au moja ya mashirika yake tanzu linamiliki hakimiliki ya uchaguaji, uratibu, mpangilio na uboreshaji wa Tovuti.
4. ALAMA ZA BIASHARA ZA COMPASSION
Alama za biashara na alama za huduma zinazotumiwa au kuonyeshwa kwenye Tovuti ("Alama za Biashara") ni alama za biashara zilizosajiliwa na ambazo hazijasajiliwa za Compassion, moja ya mashirika yake tanzu, au watu wake wa tatu. Hakuna kitu chochote kilicho kwenye Tovuti kitafasiriwa kama cha kupeanwa - kwa kidokezi, zuio, au vinginevyo - leseni au haki yoyote ya kutumia Alama zozote za Biashara zinazoonyeshwa kwenye Tovuti bila ruhusa wazi ya awali iliyoandikwa kutoka Compassion au mmiliki wa alama ya biashara, kama inavyotumika. Hasa, huwezi kutumia alama yoyote ya biashara inayoonyeshwa kwenye Tovuti kama kiungo "amilifu" bila kibali kilichoandikwa kabla kutoka kwa mmiliki wa alama ya biashara.
Unatambua kwamba Alama za Biashara zina sifa ya kipekee, inayofanya iwe vigumu kukadiria hasara ya kifedha ambayo Compassion itapata pakiwa tukio la matumizi bila idhini. Unakiri kwamba matumizi kama hayo bila idhini yatasababisha hasara kubwa kwa Compassion. Pakiwa na matumizi au ufichuzi wowote au tishio la matumizi au ufichuzi bila idhini wa Alama za Biashara, Compassion ina haki ya kupata amri ya mahakama na usaidizi wote mwingine unaofaa kutoka kwa mahakama au mamlaka yenye uwezo, bila kuhitajika: (i) kuonyesha hasara yoyote halisi au madhara yoyote halisi makubwa, (ii) kuthibitisha upungufu wa suluhisho zake za kisheria, au (iii) kutoa dhamana yoyote au usalama wowote mwingine.
5. UFIKIAJI NA MATUMIZI YA TOVUTI NA MAUDHUI
Watumiaji binafsi wa Tovuti wanaruhusiwa kupakua nakala za Maudhui yaliyo kwenye Tovuti kwa matumizi yako binafsi na sio kwa madhumuni yoyote ya kibiashara. Kwa kikomo hicho, fursa inayoweza kukanushwa ya kutumia Maudhui haianzishi uhamisho wa haki, cheo au matakwa yoyote ya Maudhui unayopakua. Huwezi, kwa hali zozote zile, (a) kurekebisha Maudhui au kuyatumia au kuyanyonya kwa madhumuni yoyote ya kibiashara, au kwa maonyesho yoyote, utendaji, uuzaji au ukodishaji wowote ule kwa umma mbali na usambazaji wenye kikomo unaohusu matumizi yako ya kibinafsi; (b) kutengua, uhandisi kinyume, au kupambua sehemu yoyote ya Tovuti au Maudhui; au (c) kuondoa hakimiliki yoyote, usajili wowote wa alama ya biashara, au notisi zingine za umiliki kutoka kwa Maudhui. Matumizi ya Maudhui yoyote au nyenzo zingine kutoka kwa Tovuti kwenye Tovuti nyingine yoyote au mazingira mengine yoyote ya kompyuta iliyo kwenye mtandao yamepigwa marufuku. Compassion ina haki ya kutekeleza haki zake za uvumbuzi kwa kiwango cha juu kisheria.
Matumizi yako ya Maudhui haya huenda yasikiuke sheria au kanuni yoyote, na wakati unatumia Tovuti, utatiii sheria zote zinazotumika za shirikisho, jimbo na za ndani ikiwa ni pamoja, bila kikomo sheria ya hakimiliki na utafuata viwango, sera na miongozo ya Compassion. Zaidi ya hayo, hutahudhurisha Compassion visivyo kwa namna yoyote ile, ikiwa ni pamoja na kama sehemu ya matumizi yoyote ya Alama za Biashara ua Maudhui na hutatumia Alama zozote za Biashara au Maudhui yoyote kwa namna ya kuchukiza au isiyo ya kufurahisha au ya kuaibisha Compassion.
6. HAKI ZILIZOHIFADHIWA
Isipokuwa haki chache za matumizi zilizotolewa kwako katika Masharti haya ya Matumizi na makubaliano yoyote mengine kati yako na Compassion, hutakuwa na haki, cheo au matakwa katika Tovuti, Alama za Biashara au Maudhui yoyote. Haki zozote ambazo hazijatolewa kabisa katika Masharti haya ya Matumizi zimehifadhiwa kabisa na Compassion. Unakiri na kukubali kwamba hupati haki zozote za umiliki kwa kupakua Maudhui yoyote kutoka kwa Tovuti. Compassion wakati mwingine, mahali popote duniani, ina haki ya kutumia au kuidhinisha watu wengine kutumia Maudhui kwa namna yoyote wanayotaka.
7. UKATIZAJI
Compassion inahifadhi haki katika hiari yake mwenyewe na kwa wakati wowote ule kukatiza au kusimamishwa na/au kuzuia ufikiaji wako kwa Tovuti au Maudhui kwa sababu yoyote ikiwa ni pamoja na, bila kikomo ikiwa umekosa kutii Masharti haya ya Matumizi au makubaliano yoyote mengine kati yako na Compassion. Unakubali kwamba Compassion haitakuwa na wajibu kwako au mtu mwingine wa tatu kwa ukatizaji au usimamishwaji au uzuiaji wa ufikiaji wako kwenye Tovuti au Maudhui.
Kwa Maudhui yoyote au Alama zozote za Biashara, Compassion itakuwa na haki ya kukatiza haki yako ya kutumia Maudhui au Alama za Biashara na kuondoa idhini iliyotolewa hapa chini ikitokea kwamba Compassion haidhibiti tena haki zinazohitajika kutoa haki hapa chini au ikitokea kwamba katika uamuzi wa biashara wa Compassion peke yake Compassion inaonelea ni vizuri kufanya hivyo.
Usimamishaji au ukatizaji wowote hautaathiri wajibu wako wa Compassion chini ya Masharti haya ya Matumizi.
8. KANUSHO
TOVUTI, MAUDHUI, ALAMA ZA BIASHARA NA TAARIFA YOTE, BIDHAA NA HUDUMA ZILIZOTOLEWA KUPITIA TOVUTI HII ZINATOLEWA KWA MISINGI YA "KAMA ILIVYO," au "INAVYOPATIKANA", BILA UWAKILISHO AU UDHIBITISHO WA AINA YOYOTE. KWA KIWANGO KINACHORUHUSIWA NA SHERIA, COMPASSION INAKANUSHA UWAKILISHO NA UTHIBITISHO WOWOTE NA WOTE, KAMA NI WA WAZI, DOKEZO, AU SHERIA ILIYOAMRIWA HALALI, KWA KUZINGATIA TOVUTI, MAUDHUI, ALAMA ZA BIASHARA NA TAARIFA, BIDHAA NA HUDUMA YOTE ILIYOTOLEWA KUPITIA TOVUTI. BILA KUPUNGUZA UJUMLA WA HAYO, COMPASSION INAKANUSHA UWAKILISHO NA UTHIBITISHO WOTE, WA WAZI, DOKEZO, AU SHERIA ILIYOAMRIWA HALALI, (A) WA MADA, KUTOKIUKA, UUZAJI NA USAWA KWA MADHUMUNI FULANI; (B) KUTOKANA NAMNA AU SHUGHULI AU NAMNA YA UTENDAJI; (C) KUHUSIANA NA USALAMA WA TOVUTI; AU (D) KWAMBA TOVUTI ITAENDESHWA BILA USUMBUFU AU HITILAFU.
SHERIA INAYOTUMIKA HAIWEZI KURUHUSU UPUNGUFU WA UTHIBITISHO FULANI, KWA HIVYO KANUSHO HILI LOTE AU SEHEMU YA KANUSHO HILI LA UTHIBITISHO HALIWEZI KUTUMIWA KWAKO.
9. KIKOMO CHA UWAJIBIKAJI
COMPASSION, AU WAFANYAKAZI, WAKURUGENZI, MAOFISA, MAAJENTI, WACHUUZI, WATOA LESENI AU WAGAWAJI WAKE WOWOTE HAWATAWAJIBIKA KWAKO AU MTU YOYOTE WA TATU KATIKA HALI YOYOTE ILE KWA HASARA INAYOTOKANA NA AU KWA UHUSIANO NA MATUMIZI YA AU KUTOWEZA KUTUMIA TOVUTI, MAUDHUI YOYOTE, ALAMA ZOZOTE ZA BIASHARA AU TAARIFA YOYOTE, BIDHAA AU HUDUMA ZOZOTE ZILIZOTOLEWA KUPITIA TOVUTI.
KIKOMO HIKI KIPANA CHA UWAJIBIKAJI KINACHOTUMIKA KWA HASARA ZOTE ZA AINA YOYOTE (IWE YA MOJA KWA MOJA, ISIYOKUWA YA MOJA KWA MOJA, YA JUMLA, MAALUM, YA KUFUATA, YA TUKIO, MFANO AU VINGINEVYO, IKIWA NI PAMOJA NA, BILA KIKOMO, HASARA YA MAPATO AU FAIDA), KAMA MADAI YANAFUATA MKATABA, KOSA LA DAAWA (IKIWA NI PAMOJA NA UZEMBE), UWAJIBIKAJI WA MASHARTI AU NADHARIA YOYOTE NYINGINE YA KISHERIA, HATA KAMA MWAKILISHI ALIYEIDHINISHWA WA COMPASSION AMESHAURIWA KUHUSU AU ANAFAA AWE ANAJUA UWEZEKANO WA HASARA KAMA HIZO, NA BILA KUZINGATIA UFANISI WA USULUHISHO MWINGINE.
IKIWA SEHEMU YOYOTE YA KIKOMO HIKI CHA UWAJIBIKAJI INABAINISHWA KUWA SIO HALALI AU HAIWEZI KUTEKELEZWA KWA SABABU YOYOTE, BASI JUMLA YA UWAJIBIKAJI WA COMPASSION (NA MTU MWINGINE YEYOTE AU SHIRIKA LINGINE LOLOTE AMBALO UWAJIBIKAJI WAKE UNGEKUWA NA KIKOMO) KWA WAJIBU AMBAO UNGEKUWA NA KIKOMO HAUTAZIDISHA DOLA TANO ($5.00).
SHERIA INAYOTUMIKA HAIWEZI KURUHUSU KIKOMO CHA UWAJIBIKAJI KILICHOWEKWA HAPA JUU, KWA HIVYO KIKOMO CHOTE CHA UWAJIBIKAJI AU SEHEMU YAKE HAKITATUMIKA KWAKO.
10. CHAGUO LA SHERIA.
Masharti haya ya Matumizi yatafasiriwa kulingana na sheria za Jimbo la Colorado bila kuzingatia kanuni zake za migongano ya sheria. Hatua au mashtaka yote yanayotokana na au yanayohusu Masharti haya ya Matumizi yatafanyika katika mahakama ya jimbo au shirikisho mjini Denver, Colorado peke yake. Kwa hivyo unakubali na kuwasilisha bila uwezo wa kukanusha kwa mamlaka ya kibinafsi ya mahakama zilizotajwa kwa madhumuni kama hayo.
11. ANUWAI
Kukosa kwa Compassion wakati wowote ule kuhitaji utendaji wa sheria yoyote ya Masharti haya ya Matumizi au kutekeleza haki yoyote iliyotolewa hapa hakutachukuliwa kama msamaha wa sheria hiyo au haki hiyo. Misamaha yote lazima iandikwe. Isipokuwa msamaha ulioandikwa una taarifa wazi ya kinyume, hakuna msamaha kutoka Compassio wa ukiukaji wowote wa sheria yoyote ya Masharti haya ya Matumizi au haki yoyote iliyotolewa hapa itafasiriwa kama msamaha wa ukiukaji wowote endelevu au unaofuata wa sheria kama hiyo, msamaha wa sheria yenyewe, au msamaha wa haki yoyote katika Masharti haya ya Matumizi. Ikiwa sheria yoyote ya Masharti haya ya Matumizi inaamuliwa na mahakama yenye mamlaka ya uwezo kinyume na sheria, sheria hiyo itabadilishwa na kufasiriwa ili kutimiza vizuri iwezavyo malengo ya sheria ya kwanza kwa kiwango cha juu kinachokubaliwa kisheria na sheria zinazosalia za Masharti haya ya Matumizi zitabakia zikitekelezwa na kutumiaka kabisa. Masharti haya ya Matumizi yana maelewano na makubaliano kamili kati yako na Compassion kuhusu Tovuti na yanazidi mawasiliano, majadiliano na makubaliano yote ya awali, yawe ya mdomo, kuandikwa, au kielektroniki kati yako na Compassion kuhusu Tovuti.