Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | Ulinzi wa Mtoto |
Mmiliki wa Rasilimali | Compassion International |
Tamko la Ahadi ya Ulinzi wa Mtoto linapinga aina zote za dhuluma na unyanyasaji wa watoto. Pia linaichochea Compassion kufanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa hakuna madhara yanayompata mtoto yeyote aliyesajiliwa katika programu kutokana na ushiriki wake kwenye huduma ya Compassion International. Kwa jinsi hiyo, waajiriwa wa Compassion, wafanyakazi wa makanisa yaliyo katika ushirikawenza na Compassion na wanaojitolea, wafanyakazi wa nchi rafiki (Global Partner) na mgeni yeyote atakayechangamana na mtoto katika programu za Compassion lazima atie saini hati ya kanuni za maadili zinazobainisha tabia inayokubalika na isiyokubalika ya watu wazima kwa watoto.
Mtandao wa ForChildren.com, unaotolewa na shirika la Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano ili kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote, jamii iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakukaribisha ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.
Mtandao wa ForChildren.com unatolewa na shirika la Compassion International, shirika lisilo la faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.