Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | Falsafa ya Mtoto |
Mmiliki wa Rasilimali | Explain Ed |
Dirisha la 4/14 linamaanisha kundi la kidemografia kuanzia umri wa miaka minne hadi miaka kumi na minne, ambalo liko wazi na ndio hupokea mambo ya kiroho na ukuaji haraka. Mungu anatuita tubadilishe tunavyowatazama watoto na kujibu umuhimu wao wa kimkakati na mahali pao pa haki katika Ufalme Wake. Wakati watu duniani wanaona watoto kama wenye ujinga na wachanga, tunaamini kwamba wana maana kwa Mungu na wanaweza kuwa maajenti wa mabadiliko katika Ufalme wa Mbinguni. Kanisa linafaa kulenga kufikia, kuwaokoa, kuwasaidia na kuwawezeisha watoto na vijana kutimiza uwezo wao kamili wa kubadilisha familia, jamii na taifa lao. Video hii ina sauti ya Kiswahili ina urefu wa dakika 2 na sekunde 58 na inafaa kwa watoto wa umri wote.
Mtandao wa ForChildren.com, unaotolewa na shirika la Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano ili kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote, jamii iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakukaribisha ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.
Mtandao wa ForChildren.com unatolewa na shirika la Compassion International, shirika lisilo la faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.