Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Category | Child Protection |
Ulinzi wa mtoto umekuwa ni jambo la kipaumbele la ushirikawenza tangu mwanzo wa huduma kwa kuwa ni
maagizo ya Mungu.Lakini Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu;wala msiwazuie;kwa
maana walio mfano wa hao,Ufalme wa mbinguni ni wao”.(Mathayo 19:14). Hivyo basi sisi wazazi wa watoto
hawa tuliopo kanisani kwa maana ya wachuangaji,watenda kazi na watu wote wanaomtumikia mtoto.
Tunapaswa kuhakikisha kuwa watoto ambao Mungu ametupa kuwatumikia wapo salama, na iwapo mtoto
anapitia mazingira ya kunyanyaswa au ana nyanyaswa taarifa za kunyanyaswa kwa mtoto huyo zinabidi
kutumwa kupitia mfumo mpya wa utoleaji wa taarifa za unyanyasaji (Resolver) na hatua stahiki kuchukuliwa
kumsaidia mtoto ambaye ni mhanga wa tukio na kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa. Kwa umuhimu huu
ndio maana tumekuja na ujumbe wa kuhamisisha maswala haya ya utoaji wa taarifa za unyanyasaji wa mtoto.
Mpendwa Mshirikamwenza,
Mungu akubariki sana kwa juhudi zako zisizo koma za kuwatetea watoto na vijana katika jamii yako.
Tuna imani katika ahadi ya Mungu kwamba “juhudi zenu si bure katika Bwana” (1 Wakorintho 15:58).
Maisha yanabadilika kupitia huduma yako na uaminifu wa wafanyakazi na watu wanaojitolea katika
kanisa lako. ASANTE kwa kuwa mtetezi wa walio hatarini katika jamii yako. ASANTE kwa kujitolea, ili
wajue thamani yao na kutiwa moyo kutafuta maisha bora ya baadaye. ASANTE kwa kile unachofanya
kila siku kuhakikisha kwamba watoto wanapata mahali salama pa kujifunza, kukua na kukutana na
upendo wa Yesu.
Tumekusanya ibada hizi zilizoandikwa na wafanyakazi wa Compassion kutoka ulimwenguni kote ili
kuwatia moyo na kukuandaa unapoendelea kuwahudumia watoto na vijana. Kila ibada inaelezea
mtazamo wa kibiblia wa maana ya kuwalinda watoto dhidi ya dhambi, kwa nini ni muhimu kwetu kama
wafuasi wa Yesu kusimama kwa niaba yao na inajumuisha maswali ya kutafakari ili kuwezesha
majadiliano Iwe utachagua kutumia ibada hizi katika mpangilio wa kikundi au kuongoza tafakari yako
binafsi na mazungumzo na Roho Mtakatifu, tunatumai utatiwa moyo. Roho wa Mungu akuimarishe
katika njia kuu.
ASANTE!
Marafiki zako wa Compassion International
ForChildren.com, presented by Compassion International, offers ideas, learning opportunities and relationships to help equip people who work with children-at-risk. We are a worldwide community of Jesus-followers who are committed to the holistic development of children. We invite you to join our collaborative community as we share with one another the ideas, experiences, methods and tools that help children thrive even in the midst of adversity.
ForChildren.com is presented by Compassion International, a registered 501(c)3 non profit organization. All resources, courses, and discussions are intended for educational use only, not for profit.