Dalili za Kiwewe
Hii ni orodha ya dalili maarufu ambazo watu huwa nazo baada ya kiwewe. Hii inaweza kuwa muhimu unapoelezea watoto au walezi jinsi kile wanachohisi (kimwili, kihisia, kiakili) kinahusiana na mambo waliyopitia awali. Watu wengi wanaamini kuwa ni wao pekee wanaohisi jinsi wanavyohisi. Inaweza kusaidia kujua kuwa hawako peke yao na dalili zao ni “hisia za kawaida kwa hali zisizo za kawaida.”
- Kusaga meno
- Tatizo la tumbo, kichefuchefu
- Maumivu ya kichwa
- Hali ya wasiwasi
- Kushindwa kujizuia kukojoa/kukojoa kitandani kwa muda mrefu
- Hali ya kutotulia
- Huzuni na kulia sana
- Msukosuko au “kuhisi kujidhuru” mara kwa mara
- Tabia ya vurugu na upinzani
- Kupoteza hamu ya kucheza
- Hali ya kuchukua tahadhari zaidi, kushiriki kwenye tabia hatari
- Tabia za kulazimisha
- Matatizo ya uhusiano (Mifano: Kujitenga au woga wa kuchangamana) Kukasirishwa haraka – kuwakaripia watu “bila sababu”
- Kutojihusisha
- Wasiwasi
- Kukosa uwezo wa kuondoa “picha akilini mwangu”
- Tatizo la kuenda kwenye eneo la ajali au tukio la kiwewe – kutotaka kurudi
- Kuwazia tukio la kiwewe – kufikiria na/au kuzungumzia kiwewe wakati wote Kurejelea yaliyopita au kumbukumbu za kudukiza, haswa ikiwa kitu kinachohusiana na tukio kinarudiwa (mtu akivaa mavazi yaleyale kama mwathiriwa, harufu iliyokuwepo kwenye tukio, kelele zilezile – kama vile ving`ora, taa zinawaka na kuzimika ghafla, n.k.)
- Kuanza woga kwa ghafla
- Kutaka kulala wakati WOTE
- Mabadiliko ya hamu ya chakula – kutohisi njaa hadi kula zaidi
- Kutengana, kukataa kutenganishwa na walezi watu wazima
- Kuogopa kulala kwenye chumba chake peke yake (hofu za usiku, majinamizi)
- Kwenda kwa yaya, kwenye kituo cha malezi ya kutwa, shule au kanisa
- Kuwa na mtu maalum
- Kuogopa giza
- Kuogopa vifaa fulani (ambavyo hakuwa akiviogopa awali)
- Kuogopa kwenda msalani au bafuni
- Kukosa kuwa imara
- Kunyonya kidole gumba
- Kupoteza hatua za ukuaji, kama vile kujisaidia haja, au kurudi nyuma kwa lugha
- Kuwa na matatizo ya kusoma
- Kuacha kuhudhuria shuleni
- Kuwa na matatizo ya kumakinika, alama za kufeli
- Kuunda michezo au mchoro unaoashiria tatizo