Tamko la Ahadi ya Ulinzi wa Matoto


Mawanda

Tamko la Ahadi ya Ulinzi wa Mtoto na Kanuni za Maadili linajumuisha matarajio yanayowahusu washirika wote marafiki wa Compassion, washirika, na wawakilishi, yaani wajumbe wote wa bodi na wafanyakazi, watu wanaojitolea, wakandarasi, na wakandarasi wadogo wa Compassion International, Inc., Nchi Fadhili, na Makanisa Washirika-wenza yote pamoja na wageni wanaohusiana moja kwa moja na walengwa.

Taarifa hii inabainisha maudhui ya msingi na ya lazima kabisa ya Tamko Rasmi la Ahadi ya Ulinzi wa Mtoto ndani ya Shirika la Kimataifa la Compassion duniani. Kanuni za maadili zinabainisha matarajio ya tabia zinazopaswa na zisizopaswa kutendeka wakati wa kuchangamana na kushirikiana na walengwa. Ofisi za Nchi na Mataifa Fadhili, wanaweza kutafsiri, kufafanua lugha, kuzingatia muktadha husika au kuongeza jambo kwenye hati hii maadamu tu Maudhui ya msingi na ya lazima kabisa yanadumishwa. Tamko la Ahadi ya Ulinzi wa Mtoto na Kanuni za Maadili linapaswa kuwa waraka wa kipekee ambao haupaswi kuunganishwa kwenye rejea nyingine au hati nyingine ya kutia sahihi.


Mamlaka

Mamlaka ya kuanzishwa kwa kanuni ya maadili na ahadi ya ulinzi wa mtoto inaweza kupatikana katika Sera ya Bodi 5.2.1 na Sera ya Menejimenti 102, "Sera ya Kimataifa ya Ulinzi wa Mtoto." Sera hizi zinaweka matarajio ya kutungwa na kuendelezwa kwa tamko la ahadi ya ulinzi wa mtoto na kanuni za maadili zinazopaswa kufuatwa na mtu yeyote anayehusika na walengwa. Kila mtu anaye saini taarifa ya Tamko la Ahadi ya Ulinzi wa Matoto na kanuni za maadili anatarajiwa kuwa na ufahamu kamili wa haya na kufuata viwango na miongozo iliyotolewa katika kanuni za maadili na tamko la ahadi ya ulinzi wamtoto. Sera ya Menejimenti pia inasema kwamba matokeo ya kukiuka kanuni za maadili na sera nyingine zinazohusiana na ulinzi wa mtoto ni pamoja na " kuchukuliwa hatua za ki-nidhamu na /au kusitisha ajira au uhusiano."


Kanuni ya Maadili

Tabia zinazotarajiwa / kukubalika

  • Nitadhihirisha heshima na utu kwa watoto wote na nitawaonyesha wao upendo na ukarimu wa Yesu bila kujali jinsi, umri, rangi, dini, usuli wa kijamii, utamaduni, mahitaji maalum au ulemavu.
  • Nitaweka matarajio sahihi na stahiki ya kuridhisha kwa watoto kulingana na umri wao na kiwango cha uwezo. (Kwa mfano, kiukuaji ni kawaida kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kuwa na hasira haraka akiwa amechoka, lakini tunatarajia kijana kutawala hisia zake hata wakati amechoka sana.)
  • Nitahusiana na walengwa kwa kuwasiliana nao kulingana na umri wao.
  • Nitawasilisha kwa mamlaka sahihi zinazohusika na kuchunguza historia ya tabia na mwenendo wangu au uchunguzi wa polisi kulingangana na sheria za nchi kabla ya kuonana uso kwa uso na walengwa (kwa kiwango cha chini - mwajiriwa anaweza kutakiwa kuleta taarifa ya uchunguzi wa historia ya tabia na mwenendo wake/uchunguzi wa polisi wakati wa kuajiriwa kwake).
  • Nitajihusisha na shughuli na walengwa katika maeneo ya wazi na ya kuonekana. na katika tukio linalohitaji eneo lisilo wazi, nitahakikisha kuwa angalau mtu mzima mmoja aliyeidhinishwa anakuwepo.
  • Kama nitashuhudia unyanyasaji wa watoto, kujua mtoto yuko katika hatari, kushuhudia tabia yoyote kwa wenzangu, washirika au wawakilishi wengine, au mtoto anakuja kwangu kutoa ripoti juu ya tukio la unyanyasaji, nitalichukua kwa uzito na kutoa taarifa kwa mfanyakazi mhusika au mamlaka husika. Nitajitahidi kufanya kila jambo lililo ndani ya uwezo zangu ili kuhakikisha mtoto anaondoka kwenye hatari.
  • Nitatunza taarifa zote juu ya uchunguzi wa unyanyasaji wa mtoto kwa siri, nitazingatia faragha na utu kwa wote wanaohusika.
  • Ikiwa nitaombwa, nitatoa ushirikiano katika uchunguzi unaohusiana na ulinzi wa mtoto na kutoa waraka wowote au taarifa nyingine zinazohitajika ili kukamilisha uchunguzi.
  • Nitachangia kujenga mazingira ambayo watoto wanaheshimiwa na kuhimizwa kujadili changamoto na haki zao.
  • Nitafuata sheria na kanuni za Compassion kuhusu mawasiliano na walengwa, ikiwa ni pamoja na mawasiliano kwa njia ya mitandao ya kijamii.
  • Nitafuata viwango vinavyosisitiza utu (kwa mfano, kurekodi tu watoto ambao wamevaa inavyopasa, wawe wanaelewa kuwa wanarekodiwa n.k) kuhusu picha ya watoto na video.
  • Nitakuwa mwangalifu juu ya mwonekano wangu, lugha, vitendo, kuhakikisha kwamba tabia yangu inaonyesha heshima kwa walengwa na familia zao, utamaduni wao na haki zao na kufuata mapendekezo yaliyotolewa.

Tabia zisizokubalika

  • Sitakuwa na uhusiano wa kimapenzi/miadi ya uchumba na kamwe sitashiriki wala kuonesha tabia zenye kuonesha matakwa ya kujamiiana/au kujamiiana na mlengwa yeyote, bila kujali umri wake
  • Sitajihusisha kamwe na tabia zenye kuonesha matakwa ya kujamiiana/au kujamiiana na mtoto yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18, bila kujali umri wa kisheria wa idhini ya kujamiana katika nchi husika
  • Sitatumia lugha ya matusi/inayoumiza hisia, inayopendekeza mambo ya kingono, ya kutweza utu, ya kudhalilisha, ya kuaibisha au isiyokubalika kwenye utamaduni wa mlengwa.
  • Sitamgusa (baadhi ya mifano ni pamoja na kumbusu, kumpapasa, kumkumbatia, kumnyayua, kumshika, nk) mlengwa kwa namna isiyofaa au kwa namna isiyokubalika katika utamaduni wake
  • Sitatumia aina yoyote ya adhabu ya kimwili (baadhi ya mifano ni pamoja na kuchapa viboko, kuzaba vibao, kulazimisha adhabu za mazoezi ya mwili, na aina nyingine za adhabu za kimwili) kama njia ya kuwarekebisha walengwa.
  • Sinta safiri peke yangu na mlengwa, bila mwakilishi aliyeidhinishwa au idhini iliyotolewa, isipokuwa katika dharura inayotishia maisha ambapo inahitajika kusafiri kwa haraka
  • Sitaajiri mtoto yeyote kwenye aina yoyote ya kazi/ajira yenye madhara kwa mtoto na nitafuata sheria za nchi kuhusu ajira za watoto
  • Kamwe sitamtembelea mlengwa, mlezi/walezi wake na / au kanisa nje ya mipaka ya programu inayokubalika au viwango vya ziara na kuwatembelea walengwa.
  • Sintakusanya, kutoa taarifa au kusaidia kutoa taarifa zinazohusu walengwa au familia zao bila kupata kwanza ruhusa inayoruhusu maudhui binafsi na ya siri kama vile hali ya afya kimwili, akili au ya kihisia, takwimu za kifedha, historia ya unyanyasaji au unyonyaji, au picha yoyote isiyokidhi viwango vya Compassion vinavyohusu utu wa mtu. Zaidi ya hayo, sitatoa taarifa ambazo zinaweza kuruhusu walengwa au familia zao kufikiwa walipo (kama ramani za kwenda nyumbani kwao, anwani zao nyumbani, au alama za kijiografia zinazoonesha eneo lao kwenye picha.) Ninaelewa kuwa kanuni hii ya kutotoa taarifa hujumuisha maudhui yaliyochapishwa katika nakala yoyote au mfumo wa kidigitali kwenye jukwaa lolote la umma au la kibinafsi.
  • Sitaunga mkono au kushiriki katika tabia isiyo ya halali, isiyo salama au ya unyanyasaji wa mtoto yeyote, ikiwa ni pamoja na unyonyaji, usafirishaji wa kibiashara, tamaduni zinazo hatarisha maisha ya mtoto, na unyanyasaji wa kiroho au mambo ya kimilia/kijadi yenye unyanyasaji.

 


Kukubali na Tamko la Ahadi

Mimi, ____________________________________, ninakubali kwamba:

  • Nimepokea nakala ya Kanuni za Maadili ya Compassion International juu ya Ulinzi wa Mtoto.
  • Ninatambua kuwa Kanuni za Maadili zina orodhesha matarajio ya Compassion International kwangu katika huduma yangu, ushiriki, na/au uhusiano wangu na Compassion International.
  • Nimesoma na kuelewa kikamilifu maudhui ya Kanuni za Maadili.
  • Nimepata mafunzo juu ya tafsiri na matumizi ya Kanuni za Maadili.
  • Nimepewa fursa ya kuuliza maswali kuhusu mambo yote ambayo sikuyaelewa.
  • Ninafahamu kuwa ikiwa nitakiuka Kanuni za Maadili basi shirika (Compassion International) linaweza kunichukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusitishiwa ajira, ushirikiano, ufadhili, na ushirikiano wowote nilionao na Compassion International.
  • Ninaelewa kuwa ukiukwaji wowote nitakaoufanya unaweza kunifanya nifunguliwe mashtaka ya kiraia na / au ya kijinai kwa mujibu wa sheria husika za nchi, pamoja na sheria za Marekani na/au Mataifa Fadhili zinazohusiana na wananchi wanaosafiri nje ya nchi.

Mimi, _________________________________________, nitajihusisha kikamilifu na kukubaliana na mambo yote yaliyomo kwenye Kanuni za Maadili ya Compassion International juu ya Ulinzi wa Mtoto zinazohusiana na huduma yangu, ajira, ushiriki, na / au uhusiano wangu na Compassion International, wafanyakazi wake, walengwa, marafiki, na washirika.